Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Abdulwahid Abu Raas, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Yemen, katika mazungumzo yake na Hans Grundberg, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, kupitia mkutano wa video, alijadili maendeleo ya hali ya ndani ya nchi na mabadiliko yaliyotokea hivi karibuni baada ya wito wa wananchi wa kuukomboa mwambao wa magharibi kutoka mikononi mwa wavamizi wanaowakandamiza na kuwadharau wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu katika mikoa ya Al-Hudaydah na Taiz. Katika mazungumzo hayo, alisisitiza msimamo thabiti wa Yemen wa kutafuta amani ya haki na kukomesha uvamizi na mzingiro uliowekwa dhidi ya Yemen.
Abu Raas alisema katika mkutano huo: “Kushughulikia kesi ya kibinadamu ni ufunguo wa kutatua kesi nyingine, na kutoshughulikia utawala wa Saudi Arabia wito wa Sana’a katika suala hili ndicho kilichosababisha hali kufikia ilipo sasa; na utawala huo ndio unaowajibika na madhara yatakayotokana na hali hiyo.”
Alizungumzia operesheni zilizotekelezwa na Vikosi vya Wanajeshi katika baadhi ya maeneo ya mwambao wa magharibi, na kusisitiza: “Hali ni thabiti, na Serikali ya Yemen inatekeleza wajibu wake wa kushughulikia hali ya kibinadamu katika maeneo hayo.”
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje pia alisisitiza: “Usafiri wa majini ni salama, na marufuku hiyo inahusu tu usafiri wa majini wa Saudi Arabia, ambao uliwekwa kabla ya matukio ya hivi karibuni.” Mwishoni, alitangaza kwamba Sana’a inaunga mkono juhudi za Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa za kufikia amani nchini Yemen.
Maoni yako